Huku dhumuni la kukutana ikiwa ni pamoja na kuzungumza ajenda mbalimbali zinazowahusu vijana, na kuelezea uzoefu wake wa uwakilishi wa vijana wa kitanzania kwenye mkutano wa kimataifa wa ushirikiano na maendeleo kwa wajasiriamali vijana. Ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa Umoja wa Kimataifa wa Chama cha Wajasiriamali Vijana / International Alliance of Young Entrepreneurs Associations (IAYEA) uliofanyika beijing, china mwaka huu mwezi wa nne. Huku Taasisi ya Jumuiya ya Vijana Wawekezaji (YIA) @yia_tanzania likiwa ni miongoni mwa washirika kwenye mkutano huo pamoja na nchi nyingine 34.
Katika mazugumzo yao pia Ndg. Mramba ametafuta fursa za ushirikiano na ubalozi wa China kufanya kazi pamoja na Taasisi ya YIA katika kuleta maendeleo chanya katika maisha ya vijana kwa kuwawezesha na kuwainua vijana katika sekta mbalimbali. Naye Mheshimiwa Balozi, Chen Mingjian ameonesha nia ya kuunga mkono juhudi kubwa zinazo fanywa na vijana wadogo wa kitanzania kutoka kwenye Taasisi yao kwa kushirikiana katika programu na miradi yao mbalimbali.
Ndg. Mramba katika mkutano huu muhimu pia aliambatana na Mjumbe wa Bodi Dkt. Rajab Rutengwe pamoja na Meneja anaeshughulikia shughuli za taasisi Ndg. Cliff Mwangosi.
